Fabregas ambeba jumla Daniella

BAADA ya kuwa kwenye uhusiano kwa miaka saba na hata kuzaa watoto, kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas hatimaye kamuoa mchumba wake, Daniella Semaan.

Fabregas alikutana na Semaan (42) kwa sasa, mwaka 2011 na kuanzisha naye uhusiano wa kimapenzi.

Kwa pamoja wamejaliwa watoto watatu ingawaje kiungo huyo alimkuta Daniella akiwa na wana wengine wawili kutokana na ndoa yake ya awali na bilionea mmoja Elie Taktouk iliyovunjika na wakaishia kutalikiana huku tajiri huyo akimshtumu Cesc kwa kumwibia mke.

Daniella alikutana na Fabregas miaka saba iliyopita katika mgahawa mmoja mjini London alipokwenda kumwombea mwanawe Joseph (aliyezaa na Tatouk) autografi. Kipindi wakikutana Daniella mwenye asili ya Lebanon alikuwa angali kwenye ndoa na Taktouk ingawaje ilikuwa yenye misukosuko.