Dogo wa Mbao FC afikiria kufuta rekodi ya Msuva

Friday August 11 2017

 

By Saddam Sadick, Mwananchi ssadic@mwananchi.co.tz

Mwanza. Straika wa timu ya Mbao FC, James Msuva amesema kuwa malengo yake katika msimu ujao wa Ligi Kuu ni kuwa mfungaji bora na kuvunja rekodi ya kaka yake, Simon Msuva.

Kinda huyo aliyejiunga na Mbao, akitokea timu ya JKT Ruvu iliyoshuka daraja, amesema kuwa kiu yake ni kuwa mfungaji bora, mchezaji bora au mchezaji bora chipukizi.

Alisema kuwa uwezo anao, isipokuwa anahitaji ushirikiano kwenye timu ili aweze kufikia malengo yake.

Pia aliongeza kuwa ndoto zake ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na kwamba atajituma zaidi ili kufikia ndoto zake.