Aipiga mnada medali kujenga ofisi ya RT

Muktasari:

  • Hatua ya mwanariadha huyo kutoa medali yake hiyo ni kuunga mkono harakati za Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday anayejiandaa kutembea kwa miguu kutoka Bagamoyo mpaka Kigoma kuchangisha fedha za ujenzi wa ofisi hizo.

Arusha. MSHINDI wa Medali wa fedha katika Mbio Fupi za Dunia za mwaka 2000 Mexico na mshindi wa kwanza na Paris Half Marathon 1999, Phaustin Baha Sulle ametangaza kuitoa medali yake hiyo ili ipigwe mnada kusaka fedha za kujenga ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Hatua ya mwanariadha huyo kutoa medali yake hiyo ni kuunga mkono harakati za Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday anayejiandaa kutembea kwa miguu kutoka Bagamoyo mpaka Kigoma kuchangisha fedha za ujenzi wa ofisi hizo.

Gidabuday alisema, Baha amemuunga mkono katika matembezi hayo kwa kuigawa medali yake hiyo ipigwe mnada kuchangisha fedha hizo, kitu ambacho kimemtia moyo, huku Baha alisema huo ni mchango wake kwa RT.

Mwanariadha huyo anakumbukwa namna mwaka 1999 alivyovuruga mbio fupi za nchini Ufaransa kabla ya kwenda kung'ara mjini Veracruz, Mexico katika mashindano hayo ya dunia ya mbio fupi akishika

nafasi ya pili.