Beki aacha ujumbe mzito Pamba FC kupanda daraja

WAKATI Beki jeuri wa  Pamba FC Meshack Kibona“Rasta” akiwa ametua tayari kwenye klabu ya Area C ya Dodoma,nyota  amewapa mchongo wa maana mabosi wa TP Lindanda ambao kama wakiufata basi watafanya kweli kwenye Daraja la Kwanza msimu ujao.

Beki huyo msimu uliopita alikipiga katika klabu ya Pamba FC kwenye Ligi Daraja la Kwanza ambapo sasa mlinzi huyo wa kati amesajiliwa na timu ya Area C ambayo iko Daraja la Pili.

 

Akizungumza na gazeti hili,Beki huyo alisema ili Pamba waweze kupanda kufanya vizuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza ni muhimu kuanza maandalizi mapema ambayo yatawasaidia kukijenga kikosi chao.

“Daraja la Kwanza ni ngumu sana hivyo ni lazima Pamba waanze maandalizi mapema  ili Mashindano yatakapoanza wawe kikosi kiwe fiti kuliko kuanza mazoezi kipindi kifupi kabla ya Ligi kuanza”alisema Rasta.

Pia alisema mabosi wa timu hiyo wanatakiwa kuboresha maslahi kwa wachezaji wao ambayo amesema itafanya nyota hao kuwa na morali ya kupambana kwenye Ligi hiyo.

 

“Wanatakiwa kuboresha maslahi ya wachezaji haswa kwenye posho hii itawapa nguvu ya kupambana uwanjani na itafanya timu ifanye vyema kwenye Ligi”alisema Beki huyo.

Akizungumzia klabu yake mpya ya Area C ,Beki huyo alisema lengo lake kubwa ni kuona timu hiyo inafanya vizuri msimu ujao na hatimaye kupanda Daraja la Kwanza.

“Nimejiunga Area C na nina malengo nayo kubwa ni kuona inapanda Daraja la Kwanza na hilo linawezekana kabisa ikiwa tu tukiwa kitu kimoja kuanzia wachezaji,mashabiki na viongozi”alisema.