Straika atamba kuilaza mapema Alliance

WINGA Raphael Siame aliyesajaliwa  na Mbao, ametamba kuiwakilisha vizuri timu hiyo katika mchezo wao dhidi ya Alliance ambao unatarajiwa kupigwa Agosti 22, katika Uwanja wa Ccm Kirumba.

Siame ambaye alikosekana katika kikosi hicho takribani wiki moja baada ya kufiwa na baba yake mzazi, amerejea katika kikosi hicho ambacho kinanolewa na kocha Amri Said.

Akizungumza  na Mwanaspoti alisema kwamba akili yake hivi sasa ameielekezea katika timu yake kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri katika Ligi Kuu.

“Nashukuru Mungu nimerejea na kuanza mazoezi na wenzangu, kikubwa nataka kuanza kufanya vizuri katika mchezo wetu huu wa kwanza kwasababu ndio unasubiliwa kwa hamu sana,” alisema.

Aliongeza kwamba anajua Viongozi wamemsajili wakiwa na matumaini makubwa nay eye, hivyo hataki kuwaangusha zaidi ya kufanya kazi yake vizuri uwanjani.