#WC2018: NUSU FAINALI: Wahuni wa England waonywa

Tuesday July 10 2018

 

London, England. Ofisa anayehusika na Usalama ndani ya Chama cha soka England, amerejea wito wa Polisi wa Uingereza, kuwaonya mashabiki wa nchi hiyo kutojihusisha na uhuni wowote wawapo nchini Russia.

Alisema FA haitawafumbia macho katika hilo, watahakikisha wanawachunguza na kuwakamata mashabiki wote watakaofanya vitendo vya kihuni katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia itakayopigwa leo ikizikutanisha England na Croatia nchini Russia.

Ofisa huyo,

hilo limetolewa baada ya mashabiki hao walioonyesha vitendo vya kihuni na kuhatarisha usalama wao wakati na baada ya mechi ya robo fainali dhidi ya Sweden.

Alisema serikali ya Uingereza chini ya waziri Mkuu, Theresa May, imeonya mara kadhaa kuhusu uhuni wa mashabiki unavyoweza kuleta maafa kwenye taifa hilo, lakini inaonekana onyo hilo limekua likipuuzwa, kutokana na mashabiki wengi kunywa pombe kupita kiasi kabla ya kwenda uwanjani.

“Hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayejihusisha kwa namna yoyote ile na ghasia nchini Russia iwe ni kabla ya mechi, wakati wa mechi au baada ya mechi, kwa hakika katika hili tutatumia kila aina ya utafiti kuwanasa wote watakaojihusisha na vurugu,” alisisitiza.