Kikosi kazi charejea Azam

WACHEZAJI ,  Himid Mao, Daniel Amour na Yakub Mohamed waliokuwa na kadi za njano, wameungana na wenzao na kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha wanaifunga Mtibwa

Sugar Jumatatu ijayo.

Wachezaji hao ambao ni tegemeo la kikosi cha kwanza, wanarudi dimbani kuisubiri klabu hiyo maarufu kwa jina la Wakatamiwa, sasa ni jukumu la kocha wao, Aristica Cioaba kuwatumia au kutowatumia.

Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema, wachezaji hao baada ya kumaliza adhabu zao,

waliungana na wenzao na sasa wanafanya mazoezi ya nguvu pamoja na wenzao kwa ajili ya mchezo huo

unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Chamazi.

"Kila kitu kinakwenda vizuri na kwa wachezaji tuliowakosa kwenye mchezo wetu uliopita kwa sababu ya kadi za njano, wameungana na wenzao na kuanza mazoezi ya nguvu,"alisema Jaffar.

Hata hivyo, wachezaji wengine ambao ni Wazir Junior aliyefiwa namama yake mzazi pamoja na Bryson

Raphael  anayeumwa,  upo uwezekano wakarejea uwanjani.