‘Cannavaro’ kuanza kazi leo

MENEJA mpya wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ bado hajaanza kazi lakini ametamka kwamba leo atakuwa kambini kuanza majukumu yake.

Akizungumza na Mwanaspoti Cannavaro alisema alishindwa kujiunga mapema na kambi ya timu hiyo kutokana na kuugua kwa mama yake mzazi.

Cannavaro alisema hata majukumu hayo yalitangazwa akiwa mbali na timu hiyo akiwa kwao Zanzibar akimuuguza mama yake na kwamba leo ataanza safari ya kuelekea kambini.

Alisema kwasasa majukumu yake bado yanafanywa na Mratibu mpya wa timu hiyo, Hafidh Saleh ambaye alikuwa akikishikilia cheo cha umeneja kabla ya uteuzi huo.

“Bado sijajiunga na timu nauguliwa na mama yangu mzazi nipo huku Zanzibar nafikiri nitajiunga na timu kesho (leo) kama mambo yataenda sawa,”alisema Cannavaro.