AY awa baba apata mtoto wa kiume

Muktasari:

  • AY ametumia ukurasa wake wa twitter kutoa taarifa hiyo ya ujio wa mtoto wao, aliyezaliwa kwenye hospitali ya Medical City Healthcare ya Texas nchini Marekani.

Dar es Salaam. Mwanamuziki Ambwenne Yessaya ‘AY’ na mkewe Rehema Sudi wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume jana.

AY ametumia ukurasa wake wa twitter kutoa taarifa hiyo ya ujio wa mtoto wao, aliyezaliwa kwenye hospitali ya Medical City Healthcare ya Texas nchini Marekani.

“Mungu ni Mwema na namshukuru sana kwa kutubariki mimi na My Beautiful Wife #Remy tarehe 12.08.2018 Medical City Healthcare Dallas Texas tumepata mtoto wa kiume AVIEL maana yake GOD IS MY FATHER.... 3.9Kgs & 27 inches...Welcome to the World AVIEL YESSAYAH ” Aliandika

 ‘AY’ na Remy walifunga ndoa Februari ya mwaka huu.