Timu hizi hazina uadui Kombe la Dunia

Timu za Denmark, Iceland na Sweden zinaonekana kuwa na urafiki wa kihistoria kutokana na kufanana utamaduni wake.

Wachambuzi wa soka wamekuwa wakihoji timu hizo zitakapokuwana zitahimili kuonyesha ubabe kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia Russia.

Timu hizo hadi sasa hazipoteza michezo yao kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea Russia.

Wananchi wake kwa nchi hizo tatu, wanafanana kuanzia kwenye lugha na  utamaduni  kwa ujumla jamabo ambalo hata wachezaji na mashabiki wanafanana kwa kila jambo.

Denmark ina mchezaji wao tegemeo anayekipiga klabu ya Tottenham, Christian Eriksen.

Wachambuzi wanahoji pindi  timu hizo tatu za zitakapokutana, zitaendeleza urafiki wao au la!