Moze Iyobo akomaa na Cookie

Monday May 14 2018

 

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam:  Ebwana, ukitaka kumkosea dansa wa msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul' Diamond', Moze Iyobo mfanyie hiki mtoto wake anayeitwa Cookie.

Iyobo ambaye amezaa mtoto huyo na Mcheza Filamu, Aunty Ezekiel ametamka wazi kuwa kati ya kitu ambacho hapendi kukiona katika maisha yake ni mtoto wake huyo awe analia.

Dansa huyo ameongea hayo kutokana na sehemu ya filamu ya Mama ni Mungu wa Dunia inayomwonyesha Cookie ambaye amecheza na mama yake Aunty kama wahusika wakuu.

"Yaani ile scene inayomuonyesha mwanangu analia, iliniumiza sana, kwa kuwa huwa sipendi kumuona Cookie wangu akilia, japo nikirudisha moyo nyuma naona si ameigiza tu, si unajua hizi kazi zao za maigizo, inanibidi nipotezea,"amesema Moze.