Mara Paap! Shilole kawafunga midomo

Muktasari:

Shilole alifunga ndoa wikiendi iliyopita na mchumba wake, Ashraf Uchebe, ikiwa ni wiki mbili kabla ya tarehe aliyoitangaza awali ya Desemba 20 ambayo kwa sasa itatumika kama ya sherehe ya tukio hilo la kihistoria kwake.

MWIMBAJI wa miondoko ya miduara nchini, Shilole, amefichua kuwa kitendo cha kufunga ndoa kwa kushtukiza ni kama kuwafunga mdomo wale waliokuwa wakimchuria kwamba hawezi kuolewa aslani.

Shilole alifunga ndoa wikiendi iliyopita na mchumba wake, Ashraf Uchebe, ikiwa ni wiki mbili kabla ya tarehe aliyoitangaza awali ya Desemba 20 ambayo kwa sasa itatumika kama ya sherehe ya tukio hilo la kihistoria kwake.

“Mimi ni mtu wa vitendo na ninapoamua kufanya jambo langu lazima liwe kweli, nimezima kelele za wale wanaonifuatilia mambo yangu na kufurahia kushindwa, hakuna aliyeamini kama nafunga ndoa na Uchebe,” alisema.

Shilole alifunga ndoa hiyo na Uchebe Desemba 6 mitaa ya Masaki, nyumbani kwa Meneja wa Diamond, Babu Tale na kuhudhuriwa na mastaa wachache, lakini msanii huyo alisema Desemba 20, sherehe babu kubwa itafanyika jijini Dar.