Kumbe JLO anapenda ubishi

Muktasari:

  • JLO amemwambia mtangazaji Jimmy Kimmel kuwa ndani yake ana ubishi uliopitiliza lakini Alex Rodriguez siku zote amekuwa mwelewa kwake.

MWANAMUZIKI Jennifer Lopez ameweka wazi kuwa licha ya tabia ya ubishi aliyonayo mpenzi wake amekuwa akimuelewa na kumchukulia jinsi alivyo.

JLO amemwambia mtangazaji Jimmy Kimmel kuwa ndani yake ana ubishi uliopitiliza lakini Alex Rodriguez siku zote amekuwa mwelewa kwake.

“Hili ni tatizo ni kweli ninalo ndani yangu nimejawa na ubishi, napenda kubishana kila kitu yaani huwa sikubali kirahisi lazima na mara zote nataka mimi nishinde lakini Rod huwa hajali hilo, mara zote ananielewa na ameshanizoea,”

JLO alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa licha ya uhusiano wao kuimarika siku hadi siku bado hajafikiria kuingia kwenye ndoa nyingine kwa kuwa anafurahia maisha yake kwa sasa.