Irene Uwoya: Kha! Kwa kipi? Mi sioni tatizo

Irene Uwoya

Muktasari:

  • Habari ya mujini kwa sasa ni Uwoya a.k.a Mrs Janjaroo, lakini jambo ambalo hulifahamu ni kuwa mwenyewe wala hana habari na ndio kwanza, anajiachia na kuwashangaa watu wanaomtolea povu.

KAMA ulikuwa hufahamu basi huko kwenye mitandao mambo ni moto kwelikweli. Ndio si Irene Uwoya kalianzisha huko na sasa watu wanatema shombo na kutokwa povu tu.

Habari ya mujini kwa sasa ni Uwoya a.k.a Mrs Janjaroo, lakini jambo ambalo hulifahamu ni kuwa mwenyewe wala hana habari na ndio kwanza, anajiachia na kuwashangaa watu wanaomtolea povu.

Iko hivi. Uwpya juzi kati kaachia kwenye ukurasa wake picha moja matata sana, akiwa ametupia kinguo kilichoacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake na ikimuonyesha akiwa anakula bata ufukweni.

Picha hizo zikawaibua watu mitandaoni ambao, walianza kutema shombo wakimshangaa ni kwani vipi mke wa mtu anaachia utamu hadharani. Baadhi ya wasanii wenzake akiwemo Shamsa Ford (Mrs Chidi Mapenzi), akanunua bifu akijaribu kumtetea sana, lakini kuna watu hawakuelewa wakamgeuzia kibao kwa shombo.

Lakini, Uwoya mwenyewe akachonga na Mwanaspoti kupitia Jarida la Jiachie na kuweka wazi kila kitu. Kwanza, alianza kwa kushangaa: “He! Kuna tatizo gani sasa, sioni shida kwani picha nilipigwa nikiwa ufukweni. Mavazi ya ufukweni hayajulikani ama wanaojadili ni wageni wa picha za ufukweni.

“Hata hiyo picha haijaanzia kwangu kwa sababu, mpiga picha wangu ndiye aliyeiweka mtandaoni, ni sehemu ya kazi yake na watu walishaanza kuiweka kwenye kurasa zao na kuijadili,” alisema Uwoya.

Hata hivyo, mzuka zaidi wa mashabiki kutema shombo kwenye mitandao, umetokana na maneno ambayo Uwoya ameandika kusindikiza picha hiyo.

Uwoya aliandika: “Ukivaa nguo za kawaida eti ana kigodoro, nikim-post mume ooh mdogo na nisipompost kwa nini humpost mara humpendi. “Nikivaa nguo za ufukweni nipo uchi mke wa mtu, sasa nasema hivi kwa wale iliyowauma poleni sana siku nyingine nitawashirikisha nikitaka kupost. Hivi kwani mimi ni wa kwanza Bongo kuvaa hivi nikiwa ufukweni. Mume wangu kaipenda balaah yaani.”

Hata hivyo, ishu ya picha hizo hazimuacha Janjaroo salama kwani, ameibuka na kuwashangaa wanamtema povu mkewe.

Janjaroo, ambaye mara kadhaa amekuwa akieleza hisia zake kwa mkewe huyo, amesema kamwe hajashtuka na hawezi kumuacha Uwoya kisa picha zinazosambaa mitandaoni.

“Sigombani na mke wangu kisa jirani kasema nigombane naye!! Hata hizo picha kusambaa sio ishu na nitazidisha mapenzi kwa kumwimbia wimbo mzuri wa mapenzi ili kuonyesha nampenda zaidi”.