Eti Mobeto anajikomba

Muktasari:

  • Hamisa na Majizo walikuwa ni wapenzi hadi kufikia hatua ya kupata mtoto wa kike, lakini baada ya muda walikuja kuachana na Majizo akahamia kwa Lulu.

WATU buana! Kitendo cha Mwanamitindo Hamisa Mobeto kuposti ujumbe katika peji yake ya Instagram kwa kuandika maneno ya kumpa pole  mwigizaji wa filamu Lulu, kwa janga alilolipata la kufungwa jela miaka miwili, eti wanasema Hamisa anajikosha ili kutaka kuyarudisha majeshi kwa Majizo ambaye anadaiwa kutoka na Lulu baada ya kumtema Hamisa.

Hamisa na Majizo walikuwa ni wapenzi hadi kufikia hatua ya kupata mtoto wa kike, lakini baada ya muda walikuja kuachana na Majizo akahamia kwa Lulu.

Sasa kutokana na watu kupenda kula Ubuyu ndio wamemtupia maneno Hamisa kuwa lengo wa ujumbe huo alioutuma katika peji yake ni kutaka kurudiana na Majizo, ukizingatia wana mgogoro na Diamond ambaye amezaa nae mtoto wa pili mwenye miezi mitatu hadi sasa.