Duma kama kajishtukia vile

Tuesday March 13 2018

 

MKALI wa Filamu Bongo, Daud Michael ‘Duma’ amesema hajakimbia Bongo na kuhamia Kenya kama baadhi ya watu wanavyozusha bali yupo nchini humo kikazi na atakapomaliza kazi yake ya kisanaa atarudi nchini na kuungana na wenzake.

“Siwezi kuhama Bongo wala kuikimbia hapa ni kwangu ni suala la utafutaji na kwa sasa mimi ndio msanii wa kimataifa, nipo Nyeri nchini kenya nikirekodi tamthilia inayoruka kwa sasa Bongo ya Nyota.”

Duma alisema alipoitwa na mtayarishaji wa tamthilia hiyo alikubalia haraka kwani lengo lake ni kwenda kuigiza Hollywood kufanya kazi na watu wa Kenya ni rahisi kumuunganisha hata na msanii mkubwa kama Lupita Nyongo, mwigizaji mkubwa kutoka Afrika ya Mashariki ambaye yupo katika filamu maarufu ya Black Panther.