Cardi B atoboa siri

Muktasari:

  • Rapa huyo amedai kuwa kuwa muda mrefu amekuwa akificha suala hilo kwa kuhofia watu wakijua huenda ikazima ndoto zake za kufanya vizuri kwenye muziki.

BAADA ya kukanusha kwa muda mrefu, hatimaye rapa, Cardi B ameweka wazi kuwa ni mjamzito.

Rapa huyo amedai kuwa kuwa muda mrefu amekuwa akificha suala hilo kwa kuhofia watu wakijua huenda ikazima ndoto zake za kufanya vizuri kwenye muziki.

Alidai kuwa hata alipofanya shoo yake Aprili 8 hofu yake kubwa ilikuwa ni watu kutambua kuwa yeye ni mjamzito.

Cardi B ameeleza hayo wakati ambao anapamba vichwa vya habari mbalimbali kufuatia mchuano wake na Nicki Minaj.

Kwa sasa rapa huyu ni miongoni mwa marapa wana otikisa kwenye miondoko ya kufoka foka.