Abdul Kiba afunga ndoa

Muktasari:

  • Lakini, kwa taarifa yako tu ni kwamba Ali na Abdu Kiba ambaye pia ni msanii wa Bongo Flava  watafanya sherehe ya pamoja Aprili 29 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Ni msimu wa ndoa tu kwenye familia ya Mzee Saleh Kiba, baada ya mdogo wa staa wa Bongo Flava, Ali Kiba, Abdu Kiba naye kufunga ndoa na mchumba wake jijini Dar es Salaam, leo. Abdul amefunga ndoa hiyo ikiwa ni siku tatu tu tangu Ali Kiba afunge ndoa na mchumba wake, Amina Khalef mjini Mombasa.

Lakini, kwa taarifa yako tu ni kwamba Ali na Abdu Kiba ambaye pia ni msanii wa Bongo Flava  watafanya sherehe ya pamoja Aprili 29 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Wakati Ali na Abdu Kiba wakivuta wenza wao, dada yao aitwaye Zabibu Kiba naye anajiandaa kufunga ndoa na mchumba wake, beki wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda. Ndoa ya Zabibu na Banda itafungwa mwezi Agosti, mwaka huu.