Ronaldo, Ramos wamemtaka Lewandowski

Muktasari:

  • Lewandowski alishudia Ronaldo akifunga mabao matatu ya utata wakati Real ikitoa Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  • Lakini kwa mujibu wa gazeti la Hispania la AS, limesema nyota hao wawili wa Madrid walitumia muda wao mwisho wa mechi hiyo kuzungumza na mshambuliaji huyo kujaribu kumshawishi ajiunge nao.

Madrid, Hispania .Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos wanajaribu kumshawishi mshambuliaji Robert Lewandowski ajiunga na Real Madrid msimu ujao.

Lewandowski alishudia Ronaldo akifunga mabao matatu ya utata wakati Real ikitoa Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini kwa mujibu wa gazeti la Hispania la AS, limesema nyota hao wawili wa Madrid walitumia muda wao mwisho wa mechi hiyo kuzungumza na mshambuliaji huyo kujaribu kumshawishi ajiunge nao.

Mshambuliaji huyo wa Poland mkataba wake wa sasa utamalizika 2021 ni moja wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika Bundesliga akipokea pauni12.5milioni kwa mwaka.

Wakati Karim Benzema akiwa na mchango wake Real, lakini Ronaldo na Ramos wamemwambia Lewandowski kuwa atakuwa na nafasi katika kikosi cha Zinedine Zidane.