Mourinho amtolea macho Dembele

Wednesday April 19 2017

 

By London, England

Jose Mourinho anataka kuichokoza Borussia Dortmund kwa kutangaza nia ya kumataka chipukizi wao Ousmane Dembele. 

Manchester United watalazimika kulipa pauni 50milioni ili kuinasa saini ya mshambuliaji huyo Mfaransa.

Dembele (19), alikataa kujiunga na Man United, Chelsea, Arsenal na klabu nyingine kubwa Ulaya na kujiunga na miamba ya Ujerumani akitokea Rennes mwaka jana.

Dembele anaamini kuna nafasi kubwa ya kucheza akiwa Dortmund, kwa sababu ya sera ya klabu hiyo ya kutoa nafasi kwa vijana kucheza kikosi cha kwanza.

Mfaransa huyo alithibisha ubora wake baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa ambao Dortmund ilifungwa 3-2 na Monaco.