Soka

Mayanga aita 24, Stars safari ya 2019, Cameroon

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kitakachoingia kambini mwisho wa mwezi huu 

By Eliya Solomon, Mwananchi esolomon@mwananchi.co.tz  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Ijumaa,Mei19  2017  saa 13:6 PM

Dar es Salaam.  Kocha wa timu ya Taifa Stars, Salum Mayanga ameita kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Afcon 2019.

Stars itaingia kambini 23, kabla ya kwenda Misri kwa kambi ya wiki moja kuanzi Mei 30, kwa lengo la kujianda na mechi dhidi ya Lesotho itakayochezwa Juni.

Tanzania imepangwa Kundi L, pamoja na Cape Verde, Uganda, na Lesotho katika kusaka kufuzu kwa fainali Cameroon 2019.

Stars itaanzia nyumbani kwa kucheza na Lesotho  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 10, kabla ya kwenda Uganda mwezi Machi 23, 2018, itawafuata Cape Verde hapo Septemba 5, 2018 na kurudiana Dar es Salaam Septemba 9.

Baada ya hapo Tanzania itakwenda Lesotho Oktoba 12, 2018 na kumaliza na Uganda Dar es Salaam Novemba 9.

Pia, kambi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya Chan 2018 nchini Kenya ambako Stars itacheza dhidi ya Rwanda jijini Dar es Salaam Julai 14 na kurudiana Julai 18.

Mshindi wa mechi hiyo Tanzania na Rwanda atacheza raundi ya tatu mshindi wa mchezo kati ya Sudan Kusini, Uganda ili kukata tiketi ya kwenda Kenya mwakani.

 

Kikosi hicho kinaundwa na makipa, Aishi  Manula (Azam), Beno Kakolanya (Yanga) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar).

 

Mabeki ni Shomari Kapombe (Azam), Hassan Ramadhani (Yanga), Mwinyi  Haji (Yanga),Mohamed  Hussein 'Tshabalala' (Simba), Salimu Abdallah (Mtibwa Sugar), Agrey Morris (Azam), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam).

 

1 | 2 Next Page»