Kloop amtosa Hart

Muktasari:

Iliripotiwa hivi karibuni kuwa klabu hiyo ya Anfield ipo tayari kutoa pauni 20milioni kufanikisha uhamisho wa kipa huyo wa Manchester City, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Torino.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amefuta uwezekano wake wa kumsajili kipa wa kimataifa wa England, Joe Hart.

Iliripotiwa hivi karibuni kuwa klabu hiyo ya Anfield ipo tayari kutoa pauni 20milioni kufanikisha uhamisho wa kipa huyo wa Manchester City, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Torino.

Hart ( 30) anategemea kuondoka City, lakini Klopp amesisitiza kuendelea kubaki na makipa wake wa sasa Simon Mignolet  na Loris Karius.

"Ni kipa mzuri mwenye uwezo wa kiwango cha juu, lakini hayupo katika mipango yetu sasa wala baadaye," alisema Klopp.