Diamond noma sana

Muktasari:

Diamond jina lake halisi ni Nassib Abdul alifichua wazo la ubunifu wa bidhaa hiyo alilianza miaka mitatu iliyopita na anashukuru kufanikisha lengo, hasa ikizingatiwa amejitengenezea jina kubwa kwenye muziki hiyo kumrahisishia kazi sokoni.

"Hii ni fursa kwa jamii kwa kuweza kujipatia ajira manukato hayo hayatauzwa na mtu mmoja pekee mtu yoyote anaweza kuzinunua kwa jumla kwenye maduka ya GSM na kwenda kuziuza anakotaka," alisema Diamond.

"Ombi langu kwa serikali ni kwamba uongozi wangu umefanya kazi kubwa mpaka biashara hii inaingia sokoni, nimeisajili na ninalipa kodi, hivyo naiomba tu serikali isaidia kuniepusha na wanyonyaji na wezi na maharamia kwa kazi hii."