Costa agoma kwenda Juventus

Muktasari:

Chelsea imeanza kuwa na hofu kuhusu mwenendo wa mshambuliaji huyo kwa sasa na kuna uwezekano wa kuondoka kutokana na kushuka kwa uwezo wake wa kufunga mabao

Diego Costa amekaa kujiunga na Juventus akisema hayuko tayari kucheza kama mshambuliaji wa pili baada ya Gonzalo Higuain.

Chelsea imeanza kuwa na hofu kuhusu mwenendo wa mshambuliaji huyo kwa sasa na kuna uwezekano wa kuondoka kutokana na kushuka kwa uwezo wake wa kufunga mabao 

Antonio Conte yuko tayari kumwachia Costa mwisho wa msimu na kutafuta mshambuliaji mwenye uwezo zaidi na ufundi zaidi.

Juventus nayo ipo mbioni kuachana na Mario Mandzukic mwisho wa msimu huu, hivyo wanatafuta mshambuliaji mwingine wa kumpa ushindani Gonzalo Higuain.

Costa aliuanza msimu huu kwa kishindo kwa kuzifumania nyavu, lakini tangu mwaka huu umeanza mabao yake yamepotea.