Nzawose, Mapanya wateka Sauti za Busara

Muktasari:

Tamasha la Sauti la Busara limefikia tamati jana kwa kushikisha wanamuziki mbalimbali duniani

Zanzibar. Msanii wa nyimbo za Asili la kabila la Wagogo, Msafiri Nzawose kutoka Dodoma amekonga nyoyo za mashabiki waliofurika kwenye kilele cha tamasha la kimataifa la Muziki la Sauti za Busara lilofikia tamati usiku leo.

katika onyesho hilo, Msafiri alipanda na bendi yake alionyeesha ujuzi wa kupiga ala za muziki la kabila hilo la Wagogo kwa ustadi mkubwa.

Miongoni mwa nyimbo alizopiga jukwaani usiku huu ni pamoja na Mishemishe, Hapa Duniani, Miamwana, Makanyegale, Inyima na nyingine ambazo zipo mpya.

Mbali ya Nzawose pia bendi ya muziki inayowajumuisha vijana Saba (7) wanaosoma chuo cha Muziki Dhow Countries Music Academy (DCMA) wajulikanao kama Mapanya Band walionyesha uwezo wao katika usiku huo.

Mapanya Band waliopanda jukwaani majira ya saa mbili usiku, vijana hao licha ya kuwa na umri mdogo, wameweza kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika kushuhudia Sauti za Busara mwaka huu.

Hata hivyo, vijana hao wameeleza kuwa, kwa sasa wana nyimbo tatu wamerekodi huku zingine zikiwa mbioni endapo watapata wadhamini.