Man United yalia Trump kuwafilisi

Muktasari:

Manchester United haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England tangu 2013.

London, England. Manchester United imemshutumu Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kuchangia kupata hasara ya pauni 29 milioni katika nusu ya kwanza ya mwaka.

Manchester United imepata hasara kubwa zaidi katika miaka nane ya karibuni hiyo ni kutokana na sera mpya za kodi za Rais Trump.

Man United ilishindwa kuingiza pauni 48.8milioni, jambo lililofanya wapate hasara ya pauni 29 milioni katika miezi sita iliyopita hadi Desemba 31, kwa mujibu wa taarifa za ripoti za fedha za klabu hiyo zilizotoka Alhamisi.

Hiyo ni hasara kubwa kwa Man United tangu ilipopata hasara ya aina hiyo katika kota ya tatu 2010 walipopoteza pauni 65.8 milioni. Katika kipindi kama hiki mwaka jana walipata faida pauni 18.7 milioni.

Klabu hiyo imeshutumu sera za kodi za Rais Trump zilizosababisha makampuni nchini Marekani kupata hasara katika jitihada za rais huyo za kujenga uchumi wan chi hiyo.

Ni makampuni mengi duniani yameathirika, japokuwa Man United wameumia zaidi kwa sababu ya kutegemea mfumo wa kodi wa Marekani.

Mkurungezi wa fedha wa klabu hiyo, Cliff Baty alisisitiza kuwa ni jambo hilo pekee lililosababisha Man United kupata hasara.

“Lakini itakuwa ni faisa kwa klabu katika siku za baadaye,' alisema Baty.