Kumbe Batambuzi mpita njia tu

Dar es Salaam. Beki wa Singida United, Shafik Batambuzi amesema uwepo katika klabu hiyo ni njia kuelea mbele zaidi katika maisha yake ya soka.

Batambuzi alisema alipofuata na Singida United hakukuwa na tabu kuwakubalia kwa sababu mimi ni mchezaji wa kulipwa, natakiwa kucheza sehemu yoyote nipata maslahi yangu.

“Natakiwa kucheza kwa kujituma zaidi ya sasa hivi ili niweze kufikia malengo yangu, naamini safari yangu ya soka bado ipo na hapa nilipo ni mpenyo wa mimi kuzidi kusogea mbele zaidi ya sasa katika soka langu,” alisema.

Akizungumzia nafasi ya ubingwa katika kikosi chake, alisema wana uwezo wa kuchukua ubingwa kutokana na jinsi ambavyo ligi inaenda, lakini wanatakiwa wapate matokeo mazuri katika kila mechi.

“Timu yetu ni nzuri sana haya matokeo tuliyoyapata dhidi ya Simba hayatufanyi tupoteze malengo yetu ya kuchukua ubingwa, bado tuna kila hali ya kusaka ubingwa kwa kupata matokeo mazuri kwenye kila mechi ambayo tunakuwa tunacheza,” alisema Batambuzi.