Ramos atibua mastaa Real Madrid

Thursday August 9 2018

 

WACHEZAJI wa Real Madrid wameripotiwa kukerwa na upendeleo anaopata nahodha wao, Sergio Ramos kwenye kikosi hicho.

Wachezaji wa timu hiyo wanadhani Ramos amekuwa akipewa upandeleo kwenye baadhi ya mambo na kufurahia maisha yake huko Los Blancos kuliko wengine kwa sababu mchezaji huyo alipewa mapumziko marefu wakati wenzake, ambao alikuwa nao kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia, Isco, Marco Asensio na Lucas Vezquez walitakiwa kurudi mapema kwenye timu yao sambamba na Dani Carvajal, lakini Ramos alipewa siku zaidi za kupumzika.

Advertisement