Pogba amtaja mshindi wa Ballon d'Or 2018

Friday October 12 2018

 

PARIS, UFARANSA. PAUL Pogba ametaja majina ya mastaa wanne ambao anaamini ndio wanaopaswa kushinda tuzo ya Ballon d'Or ya mwaka huu.
Majina ya wachezaji 30 yametajwa kwenye ushiriki wa kuwania tuzo hiyo likiwamo la kiungo huyo wa Manchester United na Ufaransa, Pogba, lakini mwenyewe anaamini kuna wachezaji wengine mahiri zaidi wanastahili kuwa washindi.
Hata hivyo, Pogba hakutaka kwenda nje ya Ufaransa na kuamini wachezaji hao wanne anaoamini wanastahili tuzo, wote ni wa Ufaransa, ambao miezi miache iliyopita walifanya mambo makubwa kwenye Kombe la Dunia 2018 na kubeba ubingwa kwa kuwachapa Croatia huko Russia.
Tuzo hizo ambazo mshindi wake atatangazwa Desemba 3 mwaka huu, Pogba amewataja N'Golo Kante wa Chelsea, kipa Hugo Lloris wa Tottenham, mshambuliaji wa Paris St Germain, Kylian Mbappe na fowadi wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann kuwa ndio wanaostahili tuzo hiyo.
Wafaransa wengine wanaoshindania tuzo hiyo ni mastaa wa Real Madrid, Raphael Varane na Karim Benzema.
"Iwe ni Grizou (Griezmann), Kylian (Mbappe) au Raph' (Varane), wote wanastahili kuliko mimi," alisema Pogba.
"Siwezi kumtaja mmoja, lakini kwa moyo wangu unavyoamini ni kwamba tuzo hiyo itakwenda kwa mmoja kati ya watu hao. Mwingine ni NG (Kante)"
Tuzo zote za Ballon d'Or tangu 2008 zimekuwa zikibebwa na ama Cristiano Ronaldo au Lionel Messi na masupastaa hao wawili wote wapo

Advertisement