Kumbe John Terry ndo kiboko yake Rooney bana!

Friday October 12 2018

 

LONDON, ENGLANND. WAYNE Rooney amefichua beki kiboko yake kati ya wote aliowahi kukumbana nao uwanjani na kumtaja John Terry kuwa ni mgumu sana, anakaba hadi anakera.
Fowadi huyo wa zamani wa Manchester United, Rooney alifichua hilo wakati alipokuwa akimpongeza Terry kwa uamuzi wake wa kustaafu soka mapema wiki iliyopita. Wawili hao walikuwa wapinzani kwenye Ligi Kuu England kwa miaka 15, lakini miaka tisa walikuwa wachezaji wa timu moja kwenye timu ya taifa ya Englannd.
Roonney kwa sasa anacheza soka lake huko Marekani na amekutana na mabeki wengi wa kati kwenye eneo analocheza na Terry ndiye beki mkorofi aliyekuwa akimsumbua uwanjani. Terry kwenye Ligi Kuu England ameshinda mataji matano na mara ya kwanza alicheza akiwa na umri wa miaka 17, Oktoba 1998. Kwenye Ligi Kuu England, Rooney na Terry hawajawahi kucheza timu moja zaidi ya kuwa wapinzani tu, hasa timu zao Man United na Chelsea zilipokuwa zikikutana.
Terry kwa sasa ni kocha msaidizi wa Aston Villa akifanya kazi chini ya Dean Smith, aliyeteuliwa hivi karibuni kuchukua nafasi ya Steve Bruce, huku mchakato huo ukimtosa Thierry

Advertisement