Oliech, Otieno waula kamati ya michezo Nairobi

Wednesday July 18 2018

 

By Fadhili Athumani

Nairobi, Kenya. Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, 'Harambee Stars', Dennis Oliech na Musa Otieno wametueliwa kuunda kamati ya watu 10, watakaosimamia maendeleo ya michezo katika kaunti ya Jiji la Nairobi.
Kwa mujibu wa Gavana wa kaunti ya Nairobi, Mike Mbuvi Sonko, jukumu la kamati hiyo itakuwa ni pamoja na kutambua, kukuza na kuendeleza vipaji vya soka pamoja na kusimamia ujenzi na uendeshaji wa miundo mbinu ya michezo katika Jiji la Nairobi na viunga vyake.
Akizungumza baada ya kutia saini na kudhinisha mswada wa marekebisho maendeleo ya michezo katika kaunti ya Nairobi, Gavana Sonko alisema: “Kamati hii itakuwa na jukumu la kuhakikidha michezo katika inapewa kipaumbele katika kaunti ya Nairobi."
Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni pamoja na Hashim Kamau, Judith Njagi, Lea Mumo Mate na wengineo. Ambapo kwa mujibu wa Sonko, ujenzi wa miundombinu ya michezo ni muhimu na katika kuhakikisha hilo linatekelezeka, kamati take itashirikiana na wakandarasi ambao tayari wako kazini.
Sonko alisema tayari zoezi la ukarabati na ujenzi wa viwanja vya michezo kwa viwango vya FIFA, katika maeneo ya Dandora, Ziwani, Woodley, Riruta na Kihumbuini, limeshaanza.

Advertisement