Felix Sunzu, Kago waleta vitu ya aina yake Simba

Mastraika wapya wa Simba, Felix Sunzu na Gervais Kago

MICHAEL MOMBURI,ARUSHA MAKALI ya mastraika wapya wa Simba, Felix Sunzu na Gervais Kago yamemfurahisha kocha wa Simba, Moses Basena ambaye amethibitisha kuwa mambo makubwa yanakuja ikiwemo kwenye mechi ya Yanga, Agosti 17 katika Ngao ya Hisani. Basena ana maana kwamba kila kitu kuanzia staili, mfumo na mbinu zitabadilika si kwenye mechi ya Yanga tu bali katika mechi zote kuanzia sasa na mazoezi anayowapa wachezaji yamewakubali. Kocha huyo ameisisitizia Mwanaspoti mjini hapa kwamba kila kitu ni kipya na mafowadi hao wapya wa kigeni akiwemo Emmanuel Okwi wa Uganda wameleta mambo mapya kikosini na wamempa wigo mpana wa kufanya atakacho. ìWachezaji wa kigeni wameongeza nguvu sana kwenye timu, kwa kuwa wana uwezo. Kama unavyoweza kuona timu imebadilika kila kitu na kuwa na kiwango cha juu zaidi,îalisema Basena. ìNi wachezaji wazoefu, wana vipaji na wanajua nini wanachokifanya ndio maana unaona wameweza kuonyesha mabadiliko ndani ya muda mfupi. ìLakini bado wanahitaji muda zaidi kuonyesha mambo yao kwa kuwa wameniahidi mambo mengi sana mazuri mpaka kwa viongozi, sasa ni muda tu unatakiwa kwa wao kuzoea mazingira mapya na kufanya kinachotakiwa, lakini sina wasiwasi wameahidi na nimeshaanza kuona kwa vitendo. ìUjio wake ndani ya Simba umebadili kabisa taswira na kuongeza nguvu zaidi, sasa hivi nina wigo mpana wa kufanya kila ninachotaka haswa kwenye ushambuliaji, wako wachezaji wengi sana wenye uwezo, ukichanganya na hawa wageni. ìNina wigo mpana sana wa kufanya maamuzi na kwa aina hii ya wachezaji wenye nguvu na uwezo pamoja na kasi ni faida kubwa sana na hatari kwa kila adui, unapokuwa na timu kama hii Simba ya sasa unakuwa huna wasiwasi. ìMambo mazuri yanakuja,îalisisitiza Basena kwa kujiamini akiwa na maana kuwa kuanzia sasa mambo ni mazuri Simba na kila kitu kipo sawa uwanjani. Basena ana mtihani mkubwa wa ëkuitia adabuí Yanga ambayo iliwanyanyasa kwenye fainali ya Kagame na kuwafunga bao 1-0. Yanga ipo mjini Khartoum, Sudan ikicheza mechi za kirafiki kujiandaa na mechi ya Simba pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara inayoanza Agosti 20. Sunzu aliiambia Mwanaspoti jana Jumatatu kuwa; ìNiko vizuri na maandalizi ni mazuri sana kuelekea mechi dhidi ya Yanga, niko tayari.î