Zari amkaba kooni Diamond buda!

Muktasari:

Na kuhusu madai ya Mondi kwamba alimchepukia na nyota wa Nigeria Mr P (Peter Okoy)  mmoja wa pacha waliounda kundi la P Square, Zari alikuwa na haya ya kusema.

HUENDA soshiolaiti Zari Hassan kulisahau penzi la Diamond Platinumz haitawahi kutokea baada yake kufunguka mengi zaidi tena hivi majuzi kuhusu uhusiano wao uliotibuka ikiwemo kukanusha kuwahi kumchepukia na msanii wa Nigeria Mr P.

Mwanzo soshiolaiti huyo kasisitiza kwamba baada ya kuwa na Diamond kwa tariban miaka minne na kuzaa naye watoto wawili, alitegemea sana kwamba ndoa yao ingeishia kudumu milele ila msanii huyo akaishia kumtenda kwa kumsaliti na michepuko.

“Nilitamani kuwa na ndoa ya kudumu na Diamond na ndani ya nafsi yake anafahamu sikuwahi kumchepukia na mwanamume yeyote,” Zari alifichua kwenye mahojiano mengine ya hivi karibuni.

Na kuhusu madai ya Mondi kwamba alimchepukia na nyota wa Nigeria Mr P (Peter Okoy)  mmoja wa pacha waliounda kundi la P Square, Zari alikuwa na haya ya kusema.

“Peter nimekutana naye hata kabla ya kukutana na Diamond na ndicho kipindi nilipopiga na yeye na hiyo ni 2011 kipindi nikiwa bado na Ivan (marehemu mumewe wa zamani). Hivyo picha hizo alizoposti akinishtumu kwa kumchepukia ni za kipindi hicho.”

Pamoja na machungu anayosema alimsababishia Diamond, anajitahidi kumsamehe na kuhakikisha kwamba haihamii kwa watoto aliozaa naye (Tiffah na Nillian)  ili wasije kumjengea chuki sik