Zahera pengo la Ajib litazibika tu Yanga

Thursday May 23 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amekiri kuondoka kwa Ibrahim Ajib ni pengo lakini haina maana kwamba hawawezi kupana nyota mwingine bora wa kuziba pengo hilo.

Ajib anatajwa kutimkia TP Mazembe mwisho wa msimu huu baada ya kumalizana na Yanga na kuzima tetesi zilizokuwa zinasambaa kwamba anaweza kujiunga na timu yake ya zamani Simba.

Zahera alisema anampango wa kusajili nyota nane kabla ajatimka kuelekea nchini kwao Congo kwaajili ya mapumziko na kujiunga na timu ya Taifa akiwa kama kocha msaidizi.

"Nitaondoka Tanzania Juni 23 saa nane usiku, lakini kabla sijatimka nitataja majina ya nyota nane niliowasajili wakiwemo nyota sita wa kigeni na wawili wazawa na pia nitaweka wazi majina ya wachezaji ambao sitakuwanaop msimu ujao,"

"Ni mapema kuwaambia kuwa ni nani na nani hawana nafasi kikosini kwangu msimu ujao kwani bado nina mchezo mmoja dhidi ya Azam FC, lakini nawahakikishia nitafuteni mara baada ya mchezo huo kilakitu nitaweka wazi," alisema Zahera.

Advertisement