Zahera abadili mlango Yanga awakwepaa Waandishi

Muktasari:

Kocha Mwinyi Zahera akiwa katika gari la Mratibu na Meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh na moja kwa moja waliukwepa mlango wa mbele na kwenda kupitia mlango wa nyuma.

Dar es Salaam. Sekeseke la kutimuliwa kwa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera lazidi kushika kasi, baada ya Mkongo huyo kutoa kali zaidi baada ya kubadili mlango wa kuingia katika ofisi za makao makuu ya klabu hiyo.

Ipo hivi baada ya Yanga kumaliza mazoezi yao katika uwanja wa Polisi, Kurasini wachezaji walikuja makao makuu na kushangaa shangaa na baadae wengine waliondoka huku wengine wakiendelea kushangaa idadi kubwa kiasi ya mashabiki waliojitokeza hapa.

Kidogo alipita Kocha Mwinyi Zahera akiwa katika gari la Mratibu na Meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh na moja kwa moja waliukwepa mlango wa mbele na kwenda kupitia mlango wa nyuma.

 

Wakati Zahera anafika nao mshambuliaji wake David Molinga na kipa Faroukh Shikhalo walikuwa wanaingia hivyo, ndipo kocha huyo alitumia upenyo huo kupita mlango wa nyuma.

Mwanaspoti lilipozunguka fasta lilikuta nyuma ambapo upo mlango huo karibu na uwanja wa mazoezi ya Kaunda lilikuta gari la Hafidh aina ya Prado likiwa limeshapaki huku wawili hao wakiwa wameshaingia ndani.