Yondani kitasa anayebebwa na rekodi bongo

Muktasari:

Ukiachana na suala la utovu wa nidhamu ambalo limekuwa likimkumba kila mara, Yondani amekuwa akiaminika anapocheza kwenye mechi ngumu hasa za watani wa jadi.

BEKI wa Yanga na timu ya Tafa, Taifa Stars, Kelvin Yondani ni mm oja kati ya wachezaji wanaotegemewa katika kuimarisha ngome ya klabu hiyo akisaidiana na Alli Mtoni, Paul Godfrey ‘Boxer’.

Lakini siku za hivi karibuni, Kocha Mwinyi Zahera ameonekana kumtumia zaidi Ali Ali kutokana na tatizo la majeruhi linaloikabili klabu hiyo kwa sasa.

Hata hivyo, katika kikosi cha Taifa Stars, Yondani amekuwa akipangwa kutengeneza ukuta sambamba na Erasto Nyoni, Mohamed Hussen, Gadiel Michael na Shomary Kapombe ambao wote wamekuwa wakifanya kazi ya kibabe kulinda lango la Juma Kaseja na Mechata Mnata. Hivi karibuni, Yondani na Nyoni walitangaza kuachana na soka la kimataifa, lakini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akabadili maamuzi ya mastaa hawa kusataafu kuichezea Taifa Stars.

Anapokuwa katika majukumu yake, Yondani hapendi utani ndio maana suala la kulamba kadi kwake sio tatizo, ili mradi afanye kile anachokiamini na kutetea chama lake kusaka ushindi. Iwe kwenye kikosi cha Taifa Stars ama Yanga, anaposimama Yondani kwenye ukuta basi hata mashabiki hushusha pumzi.

Ukiachana na suala la utovu wa nidhamu ambalo limekuwa likimkumba kila mara, Yondani amekuwa akiaminika anapocheza kwenye mechi ngumu hasa za watani wa jadi.

5- Namba ya Jezi anayovaa ndani ya kikosi cha Yanga na Taifa Stars.

1 - Kadi nyekundu aliyoonyeshwa msimu uliopita wakati Yanga ikicheza na Kagera Sugar.

15- Idadi ya misimu ya Ligi Kuu ambayo amecheza Ligi Kuu Bara.

6- Idadi ya misimu ya Ligi Kuu aliyocheza Simba tangu mwaka 2006 hadi 2011/12 na Yanga akiwa na msimu wake wa nane sasa.

7- Mataji ya Ligi Kuu ambayo amebeba, Simba akibeba matatu na Yanga manne.

1- Bao alilofunga msimu uliopita katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

1984 - Mwaka ambao alizaliwa, Yondani na sasa ametimiza miaka 35.

2006 Mwaka ambao alianza kuitumikia Simba.

2017 - Alibeba taji lake la kwanza la Ligi Kuu Bara akiwa na Simba.

2008 - Mwaka ambao aliitwa kwa mara ya kwanza Taifa Stars.

2012 Alisajiliwa na Yanga baada ya kuachana na Simba.

2013- Alikuwa beki tegemeo la Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen.