Yaya Toure amvulia kofia Sterling kwa kiwango chake Manchester City

Muktasari:

  • Sterling ni miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka PFA, nyuma ya beki wa Liverpool, Virgil van Dijk.

London, England. Nyota wa zamani wa Manchester City, Yaya Toure amemtaja Pep Guardiola kuwa nyuma ya mafanikio na kiwango cha kiungo wa Raheem Sterling kwa sasa.

Sterling yupo katika kiwango bora akiwa amefunga mabao 19 na kutengeneza 16 katika michezo yote ambayo ameichezea klabu yake ya Manchester City na timu yake ya taifa la England.

Toure anayechezea Olympiacos amesema kwa miaka mitatu alikuwa akicheza sambamba na Sterling amebaini kuwa alifanya changuo sahihi la kujiunga City akitokea Liverpool, 2015.

 "Raheem, ni mdogo wangu, alijiunga nasi pindi ambapo (Manuel) Pellegrini alikuwa kocha wetu mkuu. Alipokuja Pep ndipo Sterling alipoanza taratibu kuwa mtu mwingine.

"Pep alimpa muda wa kutosha kucheza na alimuamisha kuwa anaweza. Alipokuwa akicheza Liverpool alikuwa amejawa na hofu, pia hakuwa anatazamwa kama mchezaji muhimu mbele ya Suarez na Philippe," alisema Toure.

Sterling ni miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka PFA, nyuma ya beki wa Liverpool, Virgil van Dijk.

 Upande wake Toure, tangu aondoke Manchester City mwaka jana kwa kujiunga na miamba ya soka la Ugiriki, Olympiacos amecheza michezo miwili tu.