Yanga yapita kwa hayati Nyerere

MSAFARA wa wachezaji na viongozi wa klabu ya Yanga, leo umepita katika kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo Butiama, Mara.

Msafara huo uliongozwa na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Msolla akiwa na mabosi wengine wa klabu hiyo wakiwa wanaipa sapoti timu yao.

Awali Yanga baada ya mchezo wao dhidi ya KMC uliomalizika wakishinda 2-1 uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza waliamua kubaki mkoani humo na leo Oktoba 30 wameanza safari ya kwenda Musoma, Mara.

Wachezaji hao walikuwa wakipata mawili matatu kutoka kwa wasimamizi wa eneo hilo kisha walisali dua maalumu ya kumuombea Nyerere.

Pia, walipata wasaha wa kuzungumza na mke wa Mwalimu Nyerere, Bi Maria Nyerere na kupiga nae picha kisha wakaendelea na safari yao.

Yanga ipo safarini kwenda Mara kucheza na Biashara United mchezo utakaochezwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Karume saa 10:00 jioni.