Wayne Rooney kuagwa rasmi Wembley

Muktasari:

 

  • Kipa wa zamani wa timu hiyo, Shilton ana rekodi ya mechi 125 za England. Rooney, ambaye kwa sasa anakipiga Ligi ya MLS akiitumikia DC United, ataingia kipindi cha pili na baadaye tukio zimna la kumuaga litaendelea.

MSHAMBULIA wa England, mara zote wa Wayne Rooney amesema itakuwa kitu kigeni wake kucheza kwenye Uwanja wa Wembley mechi ya kumuaga.

Rooney 33, alistaafu kucheza kucheza soka ya kimataifa mwaka 2017, lakini itakuwa mechi yake ya 120 dhidi ya Marekani kesho Alhamisi.

Rooney alisema kuwa atafurahi kuona anaondoka kwenye Uwanja wa Wembley akiwa mwenye tabasamu.

"Kucheza kwenye Uwanja wa Wembley ni kitu ambacho sikukitarajia na ninawapongeza wote kwa kweli," alisema.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Everton amestaafu kuitumikia timu ya taifa kwa mechi 119 huku akifunga mabao 53.

Chama cha Soka England, FA, kilisema kuwa mechi dhidi ya Marekani ni nafasi kwa Rooney kujitengenezea rekodi na kubakia kwenye vitabu.

"Kama ningekuwa kwenye nafasi kama zamani, ukweli ningeipiku rekodi ya Shilton, lakini sitaweza kufanya hivyo," alisema.