Winga Alliance mzuka umepanda

Muktasari:

  • Alliance FC ilianza Ligi Kuu kwa kusuasua lakini sasa imezinduka baada ya kufikisha pointi 13 jambo ambalo limempa mzuka Winga wake Dickson Ambundo ambaye amesema wamepata nguvu mpya

WINGA machachari wa Alliance FC, Dickson Ambundo amesema mwenendo wa timu yao kwasasa  unawapa nguvu na kuamini watafanya vizuri zaidi mbele ya safari huku akitamba kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kwenye nafasi nzuri.
Alliance ambayo ndio msimu wao wa kwanza kucheza Ligi Kuu ilianza vibaya michuano hiyo ambapo sasa imefufuka baada ya kujinasua mkiani na kupanda hadi nafasi ya 15 kwa pointi13.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ambundo alisema kilichokuwa kinawasumbua ni ugeni wa Ligi pamoja na kukosa bahati kwani walikuwa wakipambana lakini walishindwa kupata matokeo mazuri.
Alisema kwa sasa mwenendo wao unawapa nguvu na kujiamini hasa mechi tatu walizocheza ambapo wamevuna pointi saba.
"Tunaenda vizuri unajua tulipambana kusaka matokeo muda mrefu ila mambo yalikuwa magumu, tutaendelea kujituma kuhakikisha mzunguko wa kwanza unamalizika tukiwa nafasi nzuri,” alisema Ambundo.
Nyota huyo mwenye bao moja na asisti nne alisema kila mchezo kwao ni kama fainali katika vita ya kujinasua nafasi za mwisho na kufikia malengo yao ya kubaki kwenye Ligi.
Aliwaomba mashabiki na wadau wa soka mkoani hapa kuendelea kuwasapoti na kuwatoa hofu kuwa Alliance haitashuka daraja isipokuwa itaendelea kutandaza kandanda safi na kuwapa raha.
“Kila mchezo kwetu ni fainali kwa sababu tulipoteza mechi nyingi kwahiyo ni lazima tupigane kwa hizi za mbele, wadau na mashabiki