Wenger afunguka ishu ya Luis Suarez

Saturday October 17 2020
wenger pic

LONDON, ENGLAND. ARSENE Wenger amefunguka kwa mara ya kwanza na kuzungumzia tukio la Arsenal lililokuwa maarufu zaidi kwenye usajili wakati ilipowapa Liverpool ofa ya Pauni 40 milioni na Pauni Moja kumsajili Luis Suarez.

Kocha huyo wa zamani wa Arsenal alimfukuzia straika huyo wa zamani wa Liverpool mwaka 2013 na aliambiwa kwamba, huko Anfield kwenye mkataba wake kimewekwa kipengele kinachohitaji kulipiwa zaidi ya Pauni 40 milioni, basi unanasa saini yake. Hapo, Arsenal ikaripotiwa kupeleka ofa ya Pauni 40,000,001 ili aje kuziba pengo la Robin van Persie aliyetimkia Manchester United.

Advertisement