Wazungu wawili wadaiwa kumteka Mo Dewji

Thursday October 11 2018

 

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Mambosasa amesema mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘MO Dewji’ ametekwa na wazungu wawili.

Kamanda Mambosasa amesema wazungu hao wameteka mfanyabiashara huyo leo asubuhi Oktoba 11, katika hotel ya Colosseum, tukio lilipotokea.

Kamanda Mambosasa kwa sasa watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

"Asubuhi ya leo wazungu wawili walikuwa na gari aina ya suff. Kulikuwa na magari mawili, gari moja lilikuwa ndani na lingine lilikuwa nje, gari la ndani liliwasha taa ghafla na lile lililokuwa nje likaingia na kwenda kupaki karibu na gari la MO Dewji lililokuwa limepaki na MO akiwa ndani ya gari hilo,"amesema Mambosasa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam. 

"Wazungu wawili wakatoka na kumbana MO Dewji baada ya kutoka ndani ya gari lake, na kisha kumpakia katika gari lao aina ya suff kisha wakaondoka naye kusikojulikana," alisema Mambosasa.

Advertisement