Wawa wala haendi RD Congo

Tuesday April 9 2019

 

By Doris Maliyaga

MASIKINI Pascal Wawa! Ukweli ni kwamba, beki huyo wa kati hatasafiri na Simba kwenda Lubumbashi, DR Congo kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Wawa ambaye aliumia dakika ya sita ya mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri lakini bado hajaanza mazoezi kutokana na maumivu ya msuli wa nyuma chini ya goti la mguu wa kushoto.

“Nategemea kuanza mazoezi timu itakaporudi Dar kwa maandalizi mengine kwa sababu bado nasikia maumivu. Hata hivyo, namshukuru Mungu naendelea vizuri maana maumivu makali ya awali yamepungua,”alisema.

Advertisement