Wawa awapaotezea vibaka waliokwapua geto lake

Muktasari:

Amesema, wezi hao wamemharibia mipango yake na kumrudisha nyuma lakini anachukulia ni sehemu ya changamoto katika maisha yake.

LICHA ya wajanja kumwingiza mjini beki wa Simba, Pascal Wawa na kumuibia nguo zake zote pamoja na pesa kiasi cha dola 1,000 ambazo ni zaidi ya Sh 2,500,000.

Jamaa huyo ambaye hivi karibuni walimpachika jina la utani ‘Sultani’ kutokana na staili yake ya unyoaji wake hana noma.

Amesema, wezi hao wamemharibia mipango yake na kumrudisha nyuma lakini anachukulia ni sehemu ya changamoto katika maisha yake.

“Wamenirudisha nyuma lakini pesa na nguo zinaweza kutafutwa zikapatikana kikubwa nipo mzima naendelea kupambana,”anasema Wawa.

Amesema, wezi hao waliingia usiku majira ya saa nane na kuiba vitu hivyo.