Watatu Chelsea mbioni kumtimka Januari

Friday November 8 2019

 

CHELSEA imedaiwa kuwa mbioni kusikiliza ofa za mastaa wake watatu katika dirisha la Januari wakiongozwa na staa wa kimataifa wa Ufaransa, Olivier Giroud, 32 ambaye hana nafasi katika kikosi cha kwanza.

Giroud anahusishwa kurudi nyumbani kwao Ufaransa lakini Chelsea pia inaweza kuachana na Pedro, 32 ambaye amekuwa akisakwa na klabu za Ligi Kuu ya China baada ya Kocha, Frank Lampard kutumia makinda zaidi katika nafasi yake.

Inafahamika kuwa Giroud na Pedro mikataba yao wolte inamalizika Juni 2020 na wataruhusiwa kuanza mazungumzo na klabu nyingine kuanzia Januari.

Girou akiwa chini ya Lampard ameanza kwenye mechi moMwingine ambaye anaweza kuondoka ni beki wa kushoto, Marcos Alonso,28 ambaye amepoteza nafasi yake kwa Emerson huku pia ikidaiwa kwamba Lampard anamsaka beki wa kushoto wa Leicester City, Ben Chilwell.

Advertisement