Wanachama Simba wajitokeza kumuombea Mo Dewji

Muktasari:

  • Wanachama wa Simba waonyesha mapenzi kwa Mo Dewji baada ya kuamua kumuombea Dua

Dar es Salaam. Wanachama wa matawi mbalimbali ya klabu Simba, wamejitokeza makao makuu ya klabu hii kumuombea Dua mlezi wao Mohammed Dewji ‘MO’.

 Dua hii inafanywa maalumu kwa Mo aliyetekwa na watu wasiojulikana jana alfajiri alipokuwa anaenda kufanya mazoezi katika Hotel ya Colosseum.

Wanachama waliojitokeza makao makuu ya klabu hii ni wa jinsia zote na rika tofauti tofauti, huku wote wakiwa na sura za huzuni ilipoanza dua majira ya saa nane na nusu mchana.

Utulivu ulikuwa umetawala kwa upande wa wamama wakiomba kimoyo moyo, huku upande wa wanaume wao wakiomba kwa kupokezana.

Baada ya kupotea kwa Bilionea huyo, Serikali inaendelea na uchunguzi kuhakikisha wanampata na kumuondoa katika mikono ya watu hao wasiojulikana.