Wajasiriamali wajiongeza Chamazi

ACHANA na mashabiki kuujaza Uwanja wa Azam Compelex huku wengine wakikosa sehemu ya kukaa katika fainali za michuano ya Chalenji kwa Wanawake baadhi yao wameona hiyo ni fursa.
 Nyomi hiyo ambayo ni mchanganyiko kwa watoto, vijana na wazee kuna wale ambao hawana habari na kuangalia burudani hiyo zaidi ya kusaka pesa.
Biashara hizo zinafanywa na rika zote ambapo watoto wanatembeza karanga, akina mama wanauza mihogo mibichi, ndizi, vitumbua na bagia, mihogo ya kukaanga, mayai na ice cream.
Wakati kuna watu wanaonekana kuchukizwa na kukosa sehemu ya kukaa wafanyabiashara hao wanafurahia ili kufanya biashara zao.
Biashara zao zinaonekana kuwa huru ambapo ni tofauti na michuano mingine inayokuwa inafanyika uwanjani hapo ambazo mara nyingi ni za Kampuni ya Azam pekee.
Wafanyabiashara hao hufanya biashara zao ndani na pembezoni mwa ukuta wa Uwanja huo.