Madaktari Spartak Moscow wapiga marufuku ngono kuihofu Liverpool

Wednesday December 6 2017

 

Maofisa wa afya katika klabu ya Spartak Moscow ya Urusi wamewapiga marufuku wachezaji wake kujihusisha kwa namna yoyote ile na mapenzi kabla ya mechi yao ya kufuzu hatua ya 16 bora leo Jumatano usiku.
Jopo la madaktari hao limefikia hatua hiyo kutokana na kazi ngumu inayoikabiri timu hiyo ili kufuzu hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Timu hiyo inahitaji angalau pointi moja ili kwenda hatua ya makundi ambapo Liverpool ipo nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua ya makundi.
Miongoni mwa madakatri wa timu hiyo, Victoria Gameeva alisema kwamba siri kubwa na pekee ya ushindi ni wachezaji hao kutojihusisha na mapenzi kabla ya mechi yao ya leo Jumatano.