Wachezaji Simba walicheza kama watoto

Muktasari:

Aussems alisema hayo baada ya timu yake kuongoza kwa mabao 3-0 kabla ya JKT kupata bao la kufuta machozi kuwa walianza kucheza mpira kwa madaha kana kwamba siyo timu kubwa ambayo inacheza ligi ya juu jambo ambalo hakufurahishwa nalo.

KATIKA mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara, Simba dhidi ya JKT Tanzania mara baada ya kumalizika kocha Patrick Aussems, amesema wachezaji wake katika dakika 20 za mwisho walicheza na kufanya vitu kama watoto.
Aussems alisema hayo baada ya timu yake kuongoza kwa mabao 3-0 kabla ya JKT kupata bao la kufuta machozi kuwa walianza kucheza mpira kwa madaha kana kwamba siyo timu kubwa ambayo inacheza ligi ya juu jambo ambalo hakufurahishwa nalo.
"Dakika 20 za mwisho tulikuwa na uwezo wa kufunga zaidi ya hayo mabao matatu, lakini tulikuwa tukifanya mzaha na masihara kama timu ya watoto jambo ambalo si sahihi,"
"Nitakaa na wachezaji wangu mazoezini ili kuwalekeza hili kwani si jambo sahihi na wala sijafurahishwa nalo kwa ukubwa wa timu yetu ilivyo na mechi ilivyokuwa tulikuwa na uwezo wa kufunga zaidi,"
"Si kama mabadiliko yaliyofanyika ndio yalichangia hilo, hapana bali nina wachezaji 30 ambao wote nawaamini na nitawatumia katika mechi zilizo mbele na mabadiliko yatakuwepo kama ambavyo ilikuwa kwenye mchezo huu," alisema Aussems.