Van der Sar kurejea Manchester United

Muktasari:

Licha ya kwamba bado ni tetesi, Van Der Sar ni ngumu kukataa ofa hiyo ya kwenda Manchester na kuendelea kusalia Ajax

KIPA Edwin Van Der Sar aliyewahi kuichezea Manchester United, ameweka wazi yupo tayari kurejea katika klabu hiyo akiwa kwenye nafasi nyingine.
Van Der Sar mabaye hivi sasa ni Mtendaji Mkuu wa klabu ya Ajax anatajwa kurejea United kwenda kuwa Mkurugenzi wa michezo.
Licha ya kwamba bado ni tetesi, Van Der Sar ni ngumu kukataa ofa hiyo na kuendelea kusalia Ajax.
Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa nchini Uholanzi, Edwin amesema hivi sasa akili yake ipo Ajax kama kutakuwa na kitu kingine hajui.
"Hatuwezi kujua lakini kwasasa mimi nipo hapa, nguvu zangu nazielekeza hapa kama kutakuwa  na lolote tusubili tuone," amesema.
Van Der Sar aliichezea Manchester United kuanzia mwaka 2005 mpaka 2011 kwa mafanikio makubwa akichukua mataji mbalimbali.